Header Ads

  • Breaking News

    Jinsi ya kufanya simu yako ya Iphone ijae chaji haraka


     Kuna wakati kuchaji simu yako ya iphone mpaka ijae kabisa inakuwa ni mthiani mkubwa sana na kwa bahati mbaya zaidi iphone nyingi hazina teknolojia ya fast charging hivyo kufanya simu yako kuchelewa sana kujaa chaji. lakini kwa kutumia njia hizi utaweza kufanya simu yako kujaa chaji kwa haraka zaidi kuliko inavyokua kawaida, Basi moja kwa moja twende tukangalie njia hizi.
    Chaji kwa Kutumia Chaji ya iPad
    Kama unayo iPad basi lazima pia utakuwa unayo chaji yake, kama unayo basi tumia chaji hiyo yenye wattage 10W au 12W kuchaji iphone yako hii itakusaidia kuliko kutumia chaji ya iPhone ambayo inatumia 5W.
    Washa Flight Mode Unapokua Unachaji Simu
    Mara nyingi simu yako ya iphone inatumia chaji kutokana na vitu mbalimbali ambavyo vinakua bado vinafanya kazi, lakini pale unapoweka Flight Mode umeme unaoingia kwenye simu yako unakuwa hautumiki kwa vyvovyote zaidi ya kuchaji battery ya simu yako, hivyo flight mode husaidia sana.
    Zima Kabisa Simu Yako Unapochaji
    Njia nyingine ni kuhakikisha unazima simu yako unapochaji, sababu zinafanana sana na hizo hapo juu kwani pale unapozima simu yako unaruhusu chaji kuingia kwenye battery pekee bila kutumika na kitu chochote ambacho kinafanya kazi pale simu yako inapokua imewashwa.
    Chaji Simu Yako Kwenye Hali ya Hewa Iliyopowa
    Hii ni muhimu sana kumbuka kuchaji simu yako kwenye hali ya hewa ambayo ina ubaridi kidogo, kwani kwa mujibu wa taarifa mbalimbali iphone ikichajiwa sehemu yenye joto kali basi uwezo wake wa kujaa chaji kwa haraka unakuwa ni mdogo sana, lakini pia kumbuka hali ya hewa kiwa baridi sana pia simu yako itakawai kujaa chaji hivyo hakikisha sehemu unayochaji simu yako iwe na hewa kidogo na sio yenye joto kupindukia au baridi kupindukia angalau (20 degrees celsius – 30 degrees celsius).
    Zima Programu Zote Ambazo Hazina umahana muda huo.


    No comments

    Post Top Ad

    Post Bottom Ad